Repository logo
Communities & Collections
All of DSpace
  • English
  • العربية
  • বাংলা
  • Català
  • Čeština
  • Deutsch
  • Ελληνικά
  • Español
  • Suomi
  • Français
  • Gàidhlig
  • हिंदी
  • Magyar
  • Italiano
  • Қазақ
  • Latviešu
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Српски
  • Svenska
  • Türkçe
  • Yкраї́нська
  • Tiếng Việt
Log In
New user? Click here to register.Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Mercy Muthoni Kariuki1*, Prof. James Onyango Ogola, PhD1 na Prof. Nabea Wendo, PhD1"

Filter results by typing the first few letters
Now showing 1 - 2 of 2
  • Results Per Page
  • Sort Options
  • No Thumbnail Available
    Item
    Tathmini ya Athari ya Utabaka na Ukengeushi Katika Tamthilia ya Kigogo
    (East African Journal of Swahili Studies, 2025-01-28) Mercy Muthoni Kariuki1*, Prof. James Onyango Ogola, PhD1 na Prof. Nabea Wendo, PhD1
    Utabaka ni hali ya kuwagawanya watu kwa misingi ya uwezo wao wa kumiliki wa mali ilhali ukengeushi ni hali ya kumfanya mtu afuate njia ambayo si nzuri kwa kumlaghai. Hali hii husababisha migogoro miongoni mwa wahusika. Tamthilia ni kipengele cha fasihi andishi kinachowasilisha ujumbe kwa kutumia mazungumzo baina ya wahusika. Tafiti za awali katika tamthilia zilishughulikia matumizi ya lugha, mandhari, na uhusika katika tamthilia. Katika kupitia tafiti na makala mengine ya awali, mwandishi hajakumbana na tafiti kuhusu masuala ya utabaka na ukengeushi katika tamthilia ya Kigogo. Hili ndilo pengo la kiusomi ambalo lilichochea utafiti huu kufanywa ili kulijaza. Makala yalinuia kutathmini athari za utabaka na ukengeushi katika tamthilia ya Kigogo iliyoandikwa na Pauline Key. Matini yalichanganuliwa kwa kutumia misingi ya nadharia ya umarx iliyoasisiwa na Karl Heinrich Marx na kuendelezwa na wataalam kama Karl Kautsky, George Plekhanov na György Lukács. Utafiti ulifanywa maktabani ambapo athari za utabaka na ukengeushi kutokana na usomaji wa kina yalidondolewa kwa minajili ya uchanganuzi na uwasilishaji kwa kutumia mihimili ya nadharia ya umarks. Tamthilia hii ilichaguliwa kimaksudi kwa sababu inaangazia athari za utabaka na ukengeushi ambayo ndiyo mada ya makala haya. Mbinu ya kimaelezo ilitumiwa katika kuwasilisha na kuchanganua data. Usomaji wa kina wa tamthilia hii ulibainisha kuwa utabaka na ukengeushi husababisha ufisadi, ukosefu wa kazi, uchafuzi wa mazingira, ukosefu wa maendeleo, mapendeleo, kufungwa kwa soko, mauji, usherati, unyakuzi wa mashamba, chuki, uvamizi na ukombozi. Makala haya yana mchango katika uchambuzi wa vitabu teule vya fasihi andishi katika kueleza maudhui ya utabaka na ukengeushi. Utafiti huu pia ulitumiwa kama mwongozo kwa wasomi wengine watakaofanya utafiti katika fasihi andishi.
  • No Thumbnail Available
    Item
    Tathmini ya Athari ya Utabaka na Ukengeushi Katika Tamthilia ya Kigogo
    (East African Journal of Swahili Studies, 2025-01-25) Mercy Muthoni Kariuki1*, Prof. James Onyango Ogola, PhD1 na Prof. Nabea Wendo, PhD1
    Utabaka ni hali ya kuwagawanya watu kwa misingi ya uwezo wao wa kumiliki wa mali ilhali ukengeushi ni hali ya kumfanya mtu afuate njia ambayo si nzuri kwa kumlaghai. Hali hii husababisha migogoro miongoni mwa wahusika. Tamthilia ni kipengele cha fasihi andishi kinachowasilisha ujumbe kwa kutumia mazungumzo baina ya wahusika. Tafiti za awali katika tamthilia zilishughulikia matumizi ya lugha, mandhari, na uhusika katika tamthilia. Katika kupitia tafiti na makala mengine ya awali, mwandishi hajakumbana na tafiti kuhusu masuala ya utabaka na ukengeushi katika tamthilia ya Kigogo. Hili ndilo pengo la kiusomi ambalo lilichochea utafiti huu kufanywa ili kulijaza. Makala yalinuia kutathmini athari za utabaka na ukengeushi katika tamthilia ya Kigogo iliyoandikwa na Pauline Key. Matini yalichanganuliwa kwa kutumia misingi ya nadharia ya umarx iliyoasisiwa na Karl Heinrich Marx na kuendelezwa na wataalam kama Karl Kautsky, George Plekhanov na György Lukács. Utafiti ulifanywa maktabani ambapo athari za utabaka na ukengeushi kutokana na usomaji wa kina yalidondolewa kwa minajili ya uchanganuzi na uwasilishaji kwa kutumia mihimili ya nadharia ya umarks. Tamthilia hii ilichaguliwa kimaksudi kwa sababu inaangazia athari za utabaka na ukengeushi ambayo ndiyo mada ya makala haya. Mbinu ya kimaelezo ilitumiwa katika kuwasilisha na kuchanganua data. Usomaji wa kina wa tamthilia hii ulibainisha kuwa utabaka na ukengeushi husababisha ufisadi, ukosefu wa kazi, uchafuzi wa mazingira, ukosefu wa maendeleo, mapendeleo, kufungwa kwa soko, mauji, usherati, unyakuzi wa mashamba, chuki, uvamizi na ukombozi. Makala haya yana mchango katika uchambuzi wa vitabu teule vya fasihi andishi katika kueleza maudhui ya utabaka na ukengeushi. Utafiti huu pia ulitumiwa kama mwongozo kwa wasomi wengine watakaofanya utafiti katika fasihi andishi.

DSpace software copyright © 2002-2026 LYRASIS

  • Privacy policy
  • End User Agreement
  • Send Feedback
Repository logo COAR Notify