Publications

Permanent URI for this collectionhttp://41.89.103.50:4000/handle/123456789/1319

Browse

Search Results

Now showing 1 - 2 of 2
  • Item
    Utambulishaji wa mada za kigaidi katika diskosi ya ugaidi katika magazeti teule ya Kenya na ya kimataifa
    (Laikipia University, 2024-08-20) Gichohi M.Kiguta (1) Ogola J. Onyango (2) Wandera S. Simwa
    Utafiti huu ulilenga kutambua mada mbalimbali zilizojitokeza katika mashambulizi ya kigaidi na kuripotiwa na wanahabari wa Kenya na wa Kimataifa katika mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya kati ya mwaka wa 2013- 2015. Sababu kuu ya kuteua kipindi hiki ni kutokana mashambulizi makuu nchini Kenya yaliyosababishwa na kundi la Al-Shabaab dhidi ya serikali ya Kenya. Mashambulizi mawili makuu yaliyotekelezwa nchini Kenya yalikuwa ni ya Westgate mjini Nairobi na katika Chuo Kikuu cha Garissa. Ili kupata data ya uchanganuzi kuhusu mada za kigaidi, magazeti mawili makuu nchini Kenya yaliteuliwa ambayo ni Daily Nation na The Standard. Gazeti la New York Times liliteuliwa kutokana na mkabala wa jukwaa la kimataifa. Jumla ya magazeti 145 yalikusanywa na nakala 102 kuteuliwa. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Ubishi iliyojikita katika nadharia ya Pragmadeiletiki ya mhakiki ubishi Houtlousser na Frans Van Eemeren. Uchanganuzi huu wa ubishi ulipitia vitengo vya kipragmatiki. Mada za kidiskosi zilihusu, ufisadi, utetezi wa haki za kibinadamu, umoja na utangamano, umwagikaji wa damu, athari za matokeo ya vita, ulipizaji kisasi, uzalendo, nafasi ya vijana katika jamii na usalama. Matokeo ya utafiti huu yalibainisha ya kuwa kulikuwepo na tofauti za kimkabala kati ya kundi la kigaidi dhidi ya serikali ya Kenya. Ilipendekezwa kuwa mada za kigaidi katika eneo la kimataifa kama vile mashambulizi ya ugaidi kati ya Waisraeli na vita vya Gaza zinastahili kutiliwa maanani katika tafiti zijazo kwa kuwa matokeo yake yangeliweza kuwa mchango mkubwa katika kuendeleza utafiti wa diskosi za kisiasa
  • Item
    Uchanganuzi wa Mikakati ya Lugha katika Diskosi ya Kigaidi katika Magazeti ya Kenya na ya Kimataifa
    (Laikipia University, 2024-08-20) Gichohi M. Kiguta1*, Ogola J. Onyango1 na Wandera S. Simwa1
    Utafiti huu ulinuiwa kuchanganulia mikakati ya lugha katika diskosi ya kigaidi kama ilivyotumiwa katika mashambulizi ya kigaidi kati ya kundi la Al-Shabaab dhidi ya serikali ya Kenya na kuripotiwa na wanahabari. Sababu kuu ya kuteua kipindi hiki ni kwamba Serikali ya Kenya na raia wake wameendelea kushuhudia mashambulizi mengi ya ugaidi ambayo yamesababisha kuzuke diskosi ya ugaidi iliyojikita katika ubishi wa kundi la ugaidi dhidi ya serikali ya Kenya. Ili kupata data ya uchanganuzi, utafiti huu ulihusu uteuzi wa diskosi ya kigaidi kupitia mashambulizi mawili makuu yaliyofanyika nchini Kenya katika duka la kibiashara la West Gate Mall mjini Nairobi na shambulio la kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa mwezi wa Aprili, 2015. Kikundi lengwa kiliteuliwa kutokana na magazeti ya Daily Nation na The Standard yaliyohusu kipindi hicho cha kihistoria. Gazeti la NewYork Times liliteuliwa kutokana na upana wa mkabala wake wa mtazamo wa kimataifa. Jumla ya magazeti 145 yalikusanywa na nakala 102 zikateuliwa za mwanzoni mwa kipindi cha miezi miwili kabla na baada ya mwaka 2013-2015. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili, ambazo ni nadharia msingi wa Diskosi Mkabala wa Historia ya Wodak iliyotumiwa kuchanganulia mkakati wa lugha katika vitengo vya unominishaji, urejelezi, ubishi, mkabala, uzidishaji na ufifizaji. Uchanganuzi wa mikakati ya lugha ulihusu matumizi ya kijazanda, semi, virai, vishazi na sentensi. Matokeo ya utafiti huu yalibainisha kuwa kulikuwako na tofauti za kimkabala zilizozua diskosi ya ubishi kati ya kundi la kigaidi dhidi ya serikali ya Kenya. Tofauti hizi zilibainishwa kupitia mikakati ya lugha na itikadi kutokana na mashambulizi ya ugaidi yaliyotekelezwa nchini Kenya