Utambulishaji wa mada za kigaidi katika diskosi ya ugaidi katika magazeti teule ya Kenya na ya kimataifa
No Thumbnail Available
Date
2024-08-20
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Laikipia University
Abstract
Utafiti huu ulilenga kutambua mada mbalimbali zilizojitokeza katika mashambulizi ya kigaidi na kuripotiwa
na wanahabari wa Kenya na wa Kimataifa katika mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya kati ya mwaka wa
2013- 2015. Sababu kuu ya kuteua kipindi hiki ni kutokana mashambulizi makuu nchini Kenya
yaliyosababishwa na kundi la Al-Shabaab dhidi ya serikali ya Kenya. Mashambulizi mawili makuu
yaliyotekelezwa nchini Kenya yalikuwa ni ya Westgate mjini Nairobi na katika Chuo Kikuu cha Garissa. Ili
kupata data ya uchanganuzi kuhusu mada za kigaidi, magazeti mawili makuu nchini Kenya yaliteuliwa
ambayo ni Daily Nation na The Standard. Gazeti la New York Times liliteuliwa kutokana na mkabala wa
jukwaa la kimataifa. Jumla ya magazeti 145 yalikusanywa na nakala 102 kuteuliwa. Utafiti huu uliongozwa na
nadharia ya Ubishi iliyojikita katika nadharia ya Pragmadeiletiki ya mhakiki ubishi Houtlousser na Frans Van
Eemeren. Uchanganuzi huu wa ubishi ulipitia vitengo vya kipragmatiki. Mada za kidiskosi zilihusu, ufisadi,
utetezi wa haki za kibinadamu, umoja na utangamano, umwagikaji wa damu, athari za matokeo ya vita,
ulipizaji kisasi, uzalendo, nafasi ya vijana katika jamii na usalama. Matokeo ya utafiti huu yalibainisha ya
kuwa kulikuwepo na tofauti za kimkabala kati ya kundi la kigaidi dhidi ya serikali ya Kenya. Ilipendekezwa
kuwa mada za kigaidi katika eneo la kimataifa kama vile mashambulizi ya ugaidi kati ya Waisraeli na vita vya
Gaza zinastahili kutiliwa maanani katika tafiti zijazo kwa kuwa matokeo yake yangeliweza kuwa mchango
mkubwa katika kuendeleza utafiti wa diskosi za kisiasa
Description
Keywords
Kimataifa, mada, magazeti, siasa, ugaidi