Changamoto Zinazokumba Shirika la Utangazaji la Uganda Katika Kukikuza Kiswahili Jijini Kampala
No Thumbnail Available
Date
2024-09-22
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Laikipia University
Abstract
Kiswahili nchini Uganda kimetumiwa tangu enzi za kabla ya ukoloni katika
tasnia mbalimbali ila bado hakijaenea kama inavyostahili. Licha ya kuwa
Uganda kuna sera, mazoea, na utaratibu wa kuendeleza Kiswahili, bado
kina wakati mgumu kupenyeza kila mahali huku baadhi ya jamii ya
Wanauganda wakibaki kuwa na mtazamo hasi kuhusu lugha hii adimu.
Tafiti za awali zilionyesha kuwa mashirika ya utangazaji ya serikali ni
muhimu sana katika kukuza lugha za mawasiliano ulimwenguni. Nchini
Uganda, mtafiti hajakumbana na utafiti unaoonyesha chanagamoto
zinazolikumba Shirika la Utangazaji la Uganda katika kukuza lugha ya
Kiswahili. Kwa hivyo utafiti huu ulinuia kutathmini changamoto
zinazokumba Shirika la Utangazaji la Uganda katika kukikuza Kiswahili
jijini Kampala. Utafiti ulitumia nadharia ya upangaji lugha kubaini hasa
jinsi shirika hilo lenye vituo kumi na moja vya redio na vinne vya
televisheni linavyokumbana na changamoto za kukuza Kiswahili katika jiji
kuu la Kampala. Kwa kutumia nadharia hiyo utafiti uliegemea sana itikadi
nne za upangaji lugha na vipengele vinne vya mchakato wa usanifishaji wa
lugha hasa kile cha uimarishaji wa lugha. Mbinu za kurekodi, mahojiano,
uchunzaji wa kushiriki na kusoma maktabani zilitumika katika kukusanya
data. Sampuli ya utafiti huu kwa jumla ilihusisha watu 30 wakiwemo
watumishi 20 wa Shirika la Utangazaji la Uganda ambapo 10 ni Waandishi
Habari za Kiswahili. Watu 10 waliosalia waliteuliwa kutoka hadhira ya
Shirika la Utangazaji la Uganda jijini Kampala. Utafiti huu uliwalenga
wasikilizaji, watazamaji, watumishi wa makao makuu ya Shirika la
Utangazaji Uganda jijini Kampala kwa vile wao ndio wadau waliochangia
kwa kufanikisha madhumuni ya utafiti huu. Utafiti huu ulibainisha kuwa
kuna wataalamu wachache katika lugha ya Kiswahili, ukosefu wa wahisani
na ufadhili, kutokuwepo kwa sera madhubuti ya uhariri kuhusu Kiswahili,
uhaba wa vitendea kazi na mitazamo hasi kwa lugha ya Kiswahili ni baadhi
ya changamoto zinazokumba shirika la Utangazaji la Uganda katika
harakati zake za kuendeleza lugha ya Kiswahili. Utafiti huu una manufaa
kwa wizara zinazoshughulika na maendeleo ya Kiswahili Uganda kwa
sababu vile utawapa mwanga kuhusu changamoto zinazolikumba Shirika
la Utangazaji la Uganda katika harakati za kukukuza Kiswahili.
Description
Keywords
Changamoto, Shirika la Utangazaji, Kukikuza Kiswahili, Kampala.