Uchanganuzi wa Mikakati ya Lugha katika Diskosi ya Kigaidi katika Magazeti ya Kenya na ya Kimataifa
No Thumbnail Available
Date
2024-08-20
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Laikipia University
Abstract
Utafiti huu ulinuiwa kuchanganulia mikakati ya lugha katika diskosi ya
kigaidi kama ilivyotumiwa katika mashambulizi ya kigaidi kati ya kundi
la Al-Shabaab dhidi ya serikali ya Kenya na kuripotiwa na wanahabari.
Sababu kuu ya kuteua kipindi hiki ni kwamba Serikali ya Kenya na raia
wake wameendelea kushuhudia mashambulizi mengi ya ugaidi ambayo
yamesababisha kuzuke diskosi ya ugaidi iliyojikita katika ubishi wa
kundi la ugaidi dhidi ya serikali ya Kenya. Ili kupata data ya uchanganuzi,
utafiti huu ulihusu uteuzi wa diskosi ya kigaidi kupitia mashambulizi
mawili makuu yaliyofanyika nchini Kenya katika duka la kibiashara la
West Gate Mall mjini Nairobi na shambulio la kigaidi katika Chuo Kikuu
cha Garissa mwezi wa Aprili, 2015. Kikundi lengwa kiliteuliwa kutokana
na magazeti ya Daily Nation na The Standard yaliyohusu kipindi hicho
cha kihistoria. Gazeti la NewYork Times liliteuliwa kutokana na upana
wa mkabala wake wa mtazamo wa kimataifa. Jumla ya magazeti 145
yalikusanywa na nakala 102 zikateuliwa za mwanzoni mwa kipindi cha
miezi miwili kabla na baada ya mwaka 2013-2015. Utafiti huu
uliongozwa na nadharia mbili, ambazo ni nadharia msingi wa Diskosi
Mkabala wa Historia ya Wodak iliyotumiwa kuchanganulia mkakati wa
lugha katika vitengo vya unominishaji, urejelezi, ubishi, mkabala,
uzidishaji na ufifizaji. Uchanganuzi wa mikakati ya lugha ulihusu
matumizi ya kijazanda, semi, virai, vishazi na sentensi. Matokeo ya
utafiti huu yalibainisha kuwa kulikuwako na tofauti za kimkabala
zilizozua diskosi ya ubishi kati ya kundi la kigaidi dhidi ya serikali ya
Kenya. Tofauti hizi zilibainishwa kupitia mikakati ya lugha na itikadi
kutokana na mashambulizi ya ugaidi yaliyotekelezwa nchini Kenya
Description
Keywords
Mikakati, Ugaidi, Magazeti, Kenya, Kimataifa