Uchanganuzi wa Mikakati ya Lugha katika Diskosi ya Kigaidi katika Magazeti ya Kenya na ya Kimataifa

dc.contributor.authorGichohi M. Kiguta1*, Ogola J. Onyango1 na Wandera S. Simwa1
dc.date.accessioned2026-02-10T09:01:04Z
dc.date.issued2024-08-20
dc.description.abstractUtafiti huu ulinuiwa kuchanganulia mikakati ya lugha katika diskosi ya kigaidi kama ilivyotumiwa katika mashambulizi ya kigaidi kati ya kundi la Al-Shabaab dhidi ya serikali ya Kenya na kuripotiwa na wanahabari. Sababu kuu ya kuteua kipindi hiki ni kwamba Serikali ya Kenya na raia wake wameendelea kushuhudia mashambulizi mengi ya ugaidi ambayo yamesababisha kuzuke diskosi ya ugaidi iliyojikita katika ubishi wa kundi la ugaidi dhidi ya serikali ya Kenya. Ili kupata data ya uchanganuzi, utafiti huu ulihusu uteuzi wa diskosi ya kigaidi kupitia mashambulizi mawili makuu yaliyofanyika nchini Kenya katika duka la kibiashara la West Gate Mall mjini Nairobi na shambulio la kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa mwezi wa Aprili, 2015. Kikundi lengwa kiliteuliwa kutokana na magazeti ya Daily Nation na The Standard yaliyohusu kipindi hicho cha kihistoria. Gazeti la NewYork Times liliteuliwa kutokana na upana wa mkabala wake wa mtazamo wa kimataifa. Jumla ya magazeti 145 yalikusanywa na nakala 102 zikateuliwa za mwanzoni mwa kipindi cha miezi miwili kabla na baada ya mwaka 2013-2015. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili, ambazo ni nadharia msingi wa Diskosi Mkabala wa Historia ya Wodak iliyotumiwa kuchanganulia mkakati wa lugha katika vitengo vya unominishaji, urejelezi, ubishi, mkabala, uzidishaji na ufifizaji. Uchanganuzi wa mikakati ya lugha ulihusu matumizi ya kijazanda, semi, virai, vishazi na sentensi. Matokeo ya utafiti huu yalibainisha kuwa kulikuwako na tofauti za kimkabala zilizozua diskosi ya ubishi kati ya kundi la kigaidi dhidi ya serikali ya Kenya. Tofauti hizi zilibainishwa kupitia mikakati ya lugha na itikadi kutokana na mashambulizi ya ugaidi yaliyotekelezwa nchini Kenya
dc.identifier.issn2707-3475
dc.identifier.urihttp://41.89.103.50:4000/handle/123456789/1333
dc.language.isoen
dc.publisherLaikipia University
dc.relation.ispartofseriesVolume 7, Issue 1, 2024
dc.subjectMikakati
dc.subjectUgaidi
dc.subjectMagazeti
dc.subjectKenya
dc.subjectKimataifa
dc.titleUchanganuzi wa Mikakati ya Lugha katika Diskosi ya Kigaidi katika Magazeti ya Kenya na ya Kimataifa
dc.typeArticle

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
Uchanganuzi wa Mikakati ya Lugha katika Diskosi ya Kigaidi katika Magazeti ya Kenya na ya Kimataifa.pdf
Size:
316.84 KB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed to upon submission
Description:

Collections