Nafasi ya Vifaa katika Kukuuza Anthroposenia katika Riwaya za Emmanuel Mbogo na Katama Mkangi: Mfano wa Bustani ya Edeni, Vipuli vya Figo, na Mafuta
No Thumbnail Available
Date
2024-08-22
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Laikipia University
Abstract
Makala haya yametathmini nafasi ya vifaa katika kukuuza anthroposenia
katika riwaya mbili za Emmanuel Mbogo: Bustani ya Edeni na Vipuli vya
Figo, na moja ya Katama Mkangi; Mafuta. Kwa jumla, anthroposenia
humlaumu binadamu pekee kama asili ya uharibifu wa mazingira
ulimwenguni. Waandishi hawa wawili wamefanikiwa kusawiri nafasi ya
vifaa katika kukuuza anthroposenia kupitia riwaya zao teule. Lengo kuu ya
makala haya lilikuwa kujadili nafasi ya vifaa katika kukuuza anthroposenia
katika riwaya tatu zilizotajwa. Riwaya hizi tatu zilisomwa na mtafiti, kisha
data iliyodhihirisha nafasi ya vifaa katika kukuuza anthroposenia
ilitongolewa mintarafu ya lengo la makala haya. Ikizingatiwa kwamba
utafiti wa makala haya ulitumia mbinu ya upekuzi-changanuzi wa
yaliyomo katika ukusanyaji data, mtafiti alichanganua data baada ya
kuyatongoa yaliyokuwamo kwa kuongozwa na baadhi ya nguzo kuu za
Nadharia ya Uhakikimazingira ili kuafiki nia ya makala. Baadhi ya nguzo
hizo ni maendeleo endelevu, utandawazi na uongozi mbaya. Deta
iliwasilishwa na kuchanganuliwa kwa njia maelezo ilhali uchanganuzi wa
data ulihusisha mbinu ya kithamano. Suala la utafiti lililonuiwa kutatuliwa
na makala haya ni kuongeza kanoni ya anthroposenia kama taaluma.
Ilibainika bayana kuwa, waandishi wa riwaya hizi tatu wamefanikiwa
kusawiri nafasi ya vifaa katika kukuuza anthroposenia kupitia matumizi ya
vifaa kama vile jaa la taka, viwanda, mvua na matope, fedha, simu na
tarakilishi, pamoja na kitanda na mafuta
Description
Keywords
Anthroposenia, Bustani ya Edeni, Kukuuza, Uhakikimazingira, Vifaa, Vipuli vya Figo