Tathmini ya Athari ya Utabaka na Ukengeushi Katika Tamthilia ya Kigogo
No Thumbnail Available
Date
2025-01-25
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
East African Journal of Swahili Studies
Abstract
Utabaka ni hali ya kuwagawanya watu kwa misingi ya uwezo wao wa
kumiliki wa mali ilhali ukengeushi ni hali ya kumfanya mtu afuate njia
ambayo si nzuri kwa kumlaghai. Hali hii husababisha migogoro miongoni
mwa wahusika. Tamthilia ni kipengele cha fasihi andishi kinachowasilisha
ujumbe kwa kutumia mazungumzo baina ya wahusika. Tafiti za awali katika
tamthilia zilishughulikia matumizi ya lugha, mandhari, na uhusika katika
tamthilia. Katika kupitia tafiti na makala mengine ya awali, mwandishi
hajakumbana na tafiti kuhusu masuala ya utabaka na ukengeushi katika
tamthilia ya Kigogo. Hili ndilo pengo la kiusomi ambalo lilichochea utafiti
huu kufanywa ili kulijaza. Makala yalinuia kutathmini athari za utabaka na
ukengeushi katika tamthilia ya Kigogo iliyoandikwa na Pauline Key. Matini
yalichanganuliwa kwa kutumia misingi ya nadharia ya umarx iliyoasisiwa
na Karl Heinrich Marx na kuendelezwa na wataalam kama Karl Kautsky,
George Plekhanov na György Lukács. Utafiti ulifanywa maktabani ambapo
athari za utabaka na ukengeushi kutokana na usomaji wa kina yalidondolewa
kwa minajili ya uchanganuzi na uwasilishaji kwa kutumia mihimili ya
nadharia ya umarks. Tamthilia hii ilichaguliwa kimaksudi kwa sababu
inaangazia athari za utabaka na ukengeushi ambayo ndiyo mada ya makala
haya. Mbinu ya kimaelezo ilitumiwa katika kuwasilisha na kuchanganua
data. Usomaji wa kina wa tamthilia hii ulibainisha kuwa utabaka na
ukengeushi husababisha ufisadi, ukosefu wa kazi, uchafuzi wa mazingira,
ukosefu wa maendeleo, mapendeleo, kufungwa kwa soko, mauji, usherati,
unyakuzi wa mashamba, chuki, uvamizi na ukombozi. Makala haya yana
mchango katika uchambuzi wa vitabu teule vya fasihi andishi katika kueleza
maudhui ya utabaka na ukengeushi. Utafiti huu pia ulitumiwa kama
mwongozo kwa wasomi wengine watakaofanya utafiti katika fasihi andishi.
Description
Keywords
Utabaka, Ukengeushi na Tamthilia