Tathmini ya Athari ya Utabaka na Ukengeushi Katika Tamthilia ya Kigogo

dc.contributor.authorMercy Muthoni Kariuki1*, Prof. James Onyango Ogola, PhD1 na Prof. Nabea Wendo, PhD1
dc.date.accessioned2026-02-10T11:45:08Z
dc.date.issued2025-01-25
dc.description.abstractUtabaka ni hali ya kuwagawanya watu kwa misingi ya uwezo wao wa kumiliki wa mali ilhali ukengeushi ni hali ya kumfanya mtu afuate njia ambayo si nzuri kwa kumlaghai. Hali hii husababisha migogoro miongoni mwa wahusika. Tamthilia ni kipengele cha fasihi andishi kinachowasilisha ujumbe kwa kutumia mazungumzo baina ya wahusika. Tafiti za awali katika tamthilia zilishughulikia matumizi ya lugha, mandhari, na uhusika katika tamthilia. Katika kupitia tafiti na makala mengine ya awali, mwandishi hajakumbana na tafiti kuhusu masuala ya utabaka na ukengeushi katika tamthilia ya Kigogo. Hili ndilo pengo la kiusomi ambalo lilichochea utafiti huu kufanywa ili kulijaza. Makala yalinuia kutathmini athari za utabaka na ukengeushi katika tamthilia ya Kigogo iliyoandikwa na Pauline Key. Matini yalichanganuliwa kwa kutumia misingi ya nadharia ya umarx iliyoasisiwa na Karl Heinrich Marx na kuendelezwa na wataalam kama Karl Kautsky, George Plekhanov na György Lukács. Utafiti ulifanywa maktabani ambapo athari za utabaka na ukengeushi kutokana na usomaji wa kina yalidondolewa kwa minajili ya uchanganuzi na uwasilishaji kwa kutumia mihimili ya nadharia ya umarks. Tamthilia hii ilichaguliwa kimaksudi kwa sababu inaangazia athari za utabaka na ukengeushi ambayo ndiyo mada ya makala haya. Mbinu ya kimaelezo ilitumiwa katika kuwasilisha na kuchanganua data. Usomaji wa kina wa tamthilia hii ulibainisha kuwa utabaka na ukengeushi husababisha ufisadi, ukosefu wa kazi, uchafuzi wa mazingira, ukosefu wa maendeleo, mapendeleo, kufungwa kwa soko, mauji, usherati, unyakuzi wa mashamba, chuki, uvamizi na ukombozi. Makala haya yana mchango katika uchambuzi wa vitabu teule vya fasihi andishi katika kueleza maudhui ya utabaka na ukengeushi. Utafiti huu pia ulitumiwa kama mwongozo kwa wasomi wengine watakaofanya utafiti katika fasihi andishi.
dc.identifier.issn2707-3475
dc.identifier.otherhttps://doi.org/10.37284/2707-3475
dc.identifier.urihttp://41.89.103.50:4000/handle/123456789/1385
dc.language.isoen
dc.publisherEast African Journal of Swahili Studies
dc.relation.ispartofseriesVolume 8, Issue 1, 2025
dc.subjectUtabaka
dc.subjectUkengeushi na Tamthilia
dc.titleTathmini ya Athari ya Utabaka na Ukengeushi Katika Tamthilia ya Kigogo
dc.typeArticle

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
Tathmini ya Athari ya Utabaka na Ukengeushi Katika Tamthilia ya Kigogo.pdf
Size:
323.56 KB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed to upon submission
Description:

Collections