Udhalilishaji wa Asasi Kuu za Kijamii katika Muziki wa Kisasa

No Thumbnail Available

Date

2024-08-20

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Laikipia University

Abstract

Muziki wa Kisasa ni mojawapo wa muziki maarufu sana kwa vijana nchini Kenya. Licha ya kuwa kitumbuizo kwa vijana, muziki huu hutumika kama nyenzo ya kuwazindua vijana ambao wako kwenye shinikizo zito kutokana na matatizo yanayowakumba katika jamii. Tangu miaka na mikaka, binadamu amekuwa akitoa hisia zake: za uchungu, kero, mafadhaiko au furaha kupitia muziki ambao husawiri mazingira yake. Mintarafu ya hayo, makala haya yalichunguza jinsi muziki wa kisasa unatumika kudhalalisha asasi kuu za kijamii ambazo badala ya kutoa suluhisho la matatitzo chungu nzima yanayowakumba vijana, asasi hizi ndizo chanzo kuu cha matatatizo hayo. Mawazo ya Jean-Francois Lyotard katika nadharia ya usasaleo kuhusu udhalilishaji wa tamaduni na asasi kuu zinazokandamiza maisha ya watu kwani haziakisi hali halisi ya maisha yalikuwa dira katika uchunguzi huu. Muundo wa utafiti huu ulikuwa wa kiuthamano na kimaelezo na ulifanyika maktabani. Data ya msingi katika utafiti huu ilikuwa nyimbo tano za Genge ambazo zilipakuliwa mtandaoni. Makala haya yanaonyesha kwamba Muziki wa Kisasa umewapa vijana jukwaa la kudhalilisha asasi kuu kama vile dini, lugha na vyombo vya dola kwani vinawasababishia vijana mahangaiko mengi. Udhalilishaji wa asasi kuu katika tungo zao umewapa vijana njia salama ya kujikomboa kutokana na mifumo ya awali ambayo haikuwapa nafasi ya kujieleza wala kuruhusu mabadiliko. Matokeo ya utafiti huu yatakuwa malighafi katika taaluma za isimu na fasihi pamoja na uchanganuzi diskosi matini Aidha matokeo ya utafiti huu yatotoa mwanga kuhusu maswala yanayowakumba vijana hivyo basi ni marejeleo muhimu kwa washika dau wote wanaobuni sera na mikakati kabambe ya kuwainua vijana ambao ni nguzo muhimu katika jamii.

Description

Keywords

Asasi kuu, muziki wa kisasa, udhalilishaji, usasaleo, vijana

Citation

Collections

Endorsement

Review

Supplemented By

Referenced By