Utambulishaji wa mada za kigaidi katika diskosi ya ugaidi katika magazeti teule ya Kenya na ya kimataifa

dc.contributor.authorGichohi M.Kiguta (1) Ogola J. Onyango (2) Wandera S. Simwa
dc.date.accessioned2026-02-10T09:03:39Z
dc.date.issued2024-08-20
dc.description.abstractUtafiti huu ulilenga kutambua mada mbalimbali zilizojitokeza katika mashambulizi ya kigaidi na kuripotiwa na wanahabari wa Kenya na wa Kimataifa katika mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya kati ya mwaka wa 2013- 2015. Sababu kuu ya kuteua kipindi hiki ni kutokana mashambulizi makuu nchini Kenya yaliyosababishwa na kundi la Al-Shabaab dhidi ya serikali ya Kenya. Mashambulizi mawili makuu yaliyotekelezwa nchini Kenya yalikuwa ni ya Westgate mjini Nairobi na katika Chuo Kikuu cha Garissa. Ili kupata data ya uchanganuzi kuhusu mada za kigaidi, magazeti mawili makuu nchini Kenya yaliteuliwa ambayo ni Daily Nation na The Standard. Gazeti la New York Times liliteuliwa kutokana na mkabala wa jukwaa la kimataifa. Jumla ya magazeti 145 yalikusanywa na nakala 102 kuteuliwa. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Ubishi iliyojikita katika nadharia ya Pragmadeiletiki ya mhakiki ubishi Houtlousser na Frans Van Eemeren. Uchanganuzi huu wa ubishi ulipitia vitengo vya kipragmatiki. Mada za kidiskosi zilihusu, ufisadi, utetezi wa haki za kibinadamu, umoja na utangamano, umwagikaji wa damu, athari za matokeo ya vita, ulipizaji kisasi, uzalendo, nafasi ya vijana katika jamii na usalama. Matokeo ya utafiti huu yalibainisha ya kuwa kulikuwepo na tofauti za kimkabala kati ya kundi la kigaidi dhidi ya serikali ya Kenya. Ilipendekezwa kuwa mada za kigaidi katika eneo la kimataifa kama vile mashambulizi ya ugaidi kati ya Waisraeli na vita vya Gaza zinastahili kutiliwa maanani katika tafiti zijazo kwa kuwa matokeo yake yangeliweza kuwa mchango mkubwa katika kuendeleza utafiti wa diskosi za kisiasa
dc.identifier.issn2663 - 9289
dc.identifier.urihttp://41.89.103.50:4000/handle/123456789/1334
dc.language.isoen
dc.publisherLaikipia University
dc.relation.ispartofseriesIssue no: 1 | Vol no: 5 | August 2024: 21-31
dc.subjectKimataifa
dc.subjectmada
dc.subjectmagazeti
dc.subjectsiasa
dc.subjectugaidi
dc.titleUtambulishaji wa mada za kigaidi katika diskosi ya ugaidi katika magazeti teule ya Kenya na ya kimataifa
dc.typeArticle

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
Utambulishaji wa mada za kigaidi katika diskosi ya ugaidi katika magazeti teule ya Kenya na ya kimataifa.pdf
Size:
666.13 KB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed to upon submission
Description:

Collections