Arki za Utaifa wa Jamii ya Akamba
No Thumbnail Available
Date
2025-01-25
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
East African Journal of Swahili Studies,
Abstract
Utaifa wa kijamii hujitokeza katika tanzu mbalimbali za sanaa. Wanadamu
hutumia fasihi yao kuendeleza utaifa wa kijamii ili kuelezea asili yao,
changamoto zinazowakabili, maadili ya kijamii, maono na ushindi wao.
Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza jinsi nyimbo pendwa za
mwanamuziki Ken wa Maria zinavyoendeleza utaifa wa jamii ya Akamba.
Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza arki za utaifa wa jamii ya
Akamba katika nyimbo pendwa teule za Ken wa Maria. Utafiti huu
uliongozwa na Nadharia ya Utaifa iliyoasisiwa na David Smith. Nadharia ya
Utaifa hueleza kwamba ili utaifa wa jamii uwepo lazima jamii hiyo iweze
kumiliki utamaduni mmoja, lugha, imani ya dini na historia. Mihimili ya
nadharia hii ndiyo iliyoelekeza utafiti huu wakati wa kukusanya, kuchanganua
na kuwasilisha data kwa kuzingatia madhumuni ya utafiti. Muundo wa utafiti
huu ni muundo elezi. Utafiti huu ulifanyiwa katika maktaba ili kupata data.
Sampuli ya kimakusudi ilitumika ili kupata nyimbo 24 ambazo zilipakuliwa
kutoka mtandao wa YouTube na Mdundo.com. Nyimbo hizi zilitafsiriwa
katika lugha ya Kiswahili kisha kuchanganuliwa ili kubainisha arki za utaifa
wa jamii ya Akamba. Data ilichanganuliwa na matokeo yake kufafanuliwa
kwa kutumia mbinu ya kimaelezo. Uwasilishaji wa data ya utafiti ulifanywa
kwa njia ya kimaelezo. Utafiti huu ulibaini kwamba kunazo arki za utaifa
katika nyimbo pendwa za Ken wa Maria kama vile utambulisho wa kiuana na
kijamii, utamaduni, historia na ikolojia. Utafiti zaidi unaweza kufanywa
kuhusiana na mada hii hasa jinsi wasanii wengine kutoka jamii ya Akamba
wanavyotalii suala la ujenzi wa utaifa wa jamii.
Description
Keywords
Utaifa, Taifa, Utaifa wa Kijamii, Arki za Utaifa, Nyimbo Pendwa, Utamaduni, Utambulisho