Tashtiti Katika Vibonzo Vya Kisiasa: Uchunguzi Wa Vibonzo Katika Tovuti Ya Msanii Gado

dc.contributor.authorWanjiku, Mburu Kerryann.
dc.date.accessioned2025-12-09T10:17:06Z
dc.date.issued2024-10
dc.description.abstractmkubwa kwa watafiti wengi kutokana na uwezo wake wa kusimba jumbe zisizoweza kusemwa wazi wazi. Kwa kawaida, ufasiri wa vibonzo unaweza kuzua utata kutokana na sababu kadhaa. Kwanza, hadhira inaweza kufasiri ujumbe uliopo kwenye vibonzo tofauti na alivyokusudia mchora vibonzo. Pili, katika uchoraji wa vibonzo, mchora vibonzo huchukulia kuwa hadhira yake ina ujuzi wa awali kuhusiana na kinachoangaziwa. Hivyo basi, ikiwa hadhira ya mchora vibonzo haina ujuzi wa awali kuhusiana na kinachosawiriwa, huenda hadhira lengwa isipate ujumbe kama ilivyokusudiwa. Ifahamike kuwa sifa kuu ya vibonzo vya kisiasa ni kuwa vinapaswa kuwa cheshi na vyenye tashtiti ndiposa viweze kuwasilisha masuala tata kwa njia ya kimzaha. Kutokana na hali hii, utafiti huu ulichunguza tashtiti katika vibonzo vya kisiasa vya Godfrey Mwampembwa almaarufu Gado vilivyochapishwa katika mwaka wa 2017 kwenye tovuti yake. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchanganua maudhui ya kitashtiti katika vibonzo vya Gado, kisha kuhakiki mikakati iliyotumika katika kuendeleza maudhui ya kitashtiti katika vibonzo vilivyoteuliwa. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Semiotiki iliyoasisiwa na Ferdinand De Saussure, Roland Barthes na baadaye kuhakikiwa na Wamitila. Mihimili ya nadharia hii ilitumika kuchambua mikakati iliyotumiwa na Gado katika vibonzo vyake kwa minajili ya kuendeleza maudhui ya kitashtiti. Utafiti huu ni wa kimaelezo na ulifanyika mtandaoni, pale ambapo mtafiti alipekua tovuti ya Gado (www.gadocartoons.com) na kuteua kimaksudi vibonzo ishirini kutokana na jumla ya vibonzo sitini vilivyokuwa vimechapishwa katika mwaka wa 2017. Uteuzi huu ulijikita katika vibonzo vilivyofungamana na madhumuni ya utafiti huu na vilitumika kama data ya utafiti wenyewe. Baadaye, mtafiti alirekodi data aliyokusanya kwa njia ya maandishi, akaitafsiri, akaisimba na kisha kuichanganua kwa njia ya maelezo. Ufafanuzi wa matokeo ya utafiti huu ulifanywa kwa kuzingatia malengo ya utafiti, mihimili ya nadharia iliyoteuliwa na mipaka ya utafiti wenyewe. Kwa jumla, utafiti huu ulithibitisha kuwa maudhui yaliyojitokeza katika vibonzo vya Gado yalikuwa ya kitashtiti kwani yalilenga kuweka wazi maovu yaliyokuwa yakiendelezwa na serikali ya mwaka wa 2017. Waaidha, mtafiti aligundua kuwa mwanavibonzo Gado alitumia mbinu za lugha kama vile; kinaya, kejeli, metonimia, sitiara, analojia na mwingiliano matini kama mikakati ya kuibua kitashtiti katika vibonzo vyake. Vilevile, utafiti huu ulionyesha kuwa Gado alitumia ishara kama vile; matumizi ya rangi mbalimbali, pamoja na alama kama vile; heshtegi, mviringo na nyota, matumizi ya anwani na vipovu vya sauti kama mikakati ya kuibua tashtiti katika vibonzo vyake. Mwishowe, utafiti huu ulidhibitisha kuwa vibonzo vilivyochapishwa kwenye mtandao, vilidhihirisha uhuru na ukali mwingi katika usawiri wa masuala mbalimbali, jambo ambalo lilisaidia katika kufanikisha lengo kuu la tashtiti; ambalo ni ushambulizi unaochochea mabadiliko. Mwishowe, matokeo ya utafiti huu yalitarajiwa kuwanufaisha wanamawasiliano, wanasemiotiki na wasomi wa masuala ya kisiasa kwa kuwapa mtazamo mpya kuhusiana na matumizi ya maneno na ishara katika kusimba jumbe tata zinazochapishwa kwenye mtandao ambapo kuna uhuru mwingi wa kuelezea masuala tata bila kudhibitiwa.
dc.identifier.urihttp://41.89.103.50:4000/handle/123456789/84
dc.language.isoother
dc.publisherLaikipia University
dc.titleTashtiti Katika Vibonzo Vya Kisiasa: Uchunguzi Wa Vibonzo Katika Tovuti Ya Msanii Gado
dc.typeThesis

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
1_FORMATTED2-FINAL THESIS FOR KERRYANN MBURU OCTOBER 2024.pdf
Size:
3.69 MB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed to upon submission
Description: