Josephine Kanini Munyao1*, Prof. Wendo Nabea, PhD1 na Dkt. Pamela Sheila Wandera, PhD12026-02-102025-01-252707-3475https://doi.org/10.37284/jammk.8.1.2646http://41.89.103.50:4000/handle/123456789/1381Utaifa wa kijamii hujitokeza katika tanzu mbalimbali za sanaa. Wanadamu hutumia fasihi yao kuendeleza utaifa wa kijamii ili kuelezea asili yao, changamoto zinazowakabili, maadili ya kijamii, maono na ushindi wao. Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza jinsi nyimbo pendwa za mwanamuziki Ken wa Maria zinavyoendeleza utaifa wa jamii ya Akamba. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza arki za utaifa wa jamii ya Akamba katika nyimbo pendwa teule za Ken wa Maria. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Utaifa iliyoasisiwa na David Smith. Nadharia ya Utaifa hueleza kwamba ili utaifa wa jamii uwepo lazima jamii hiyo iweze kumiliki utamaduni mmoja, lugha, imani ya dini na historia. Mihimili ya nadharia hii ndiyo iliyoelekeza utafiti huu wakati wa kukusanya, kuchanganua na kuwasilisha data kwa kuzingatia madhumuni ya utafiti. Muundo wa utafiti huu ni muundo elezi. Utafiti huu ulifanyiwa katika maktaba ili kupata data. Sampuli ya kimakusudi ilitumika ili kupata nyimbo 24 ambazo zilipakuliwa kutoka mtandao wa YouTube na Mdundo.com. Nyimbo hizi zilitafsiriwa katika lugha ya Kiswahili kisha kuchanganuliwa ili kubainisha arki za utaifa wa jamii ya Akamba. Data ilichanganuliwa na matokeo yake kufafanuliwa kwa kutumia mbinu ya kimaelezo. Uwasilishaji wa data ya utafiti ulifanywa kwa njia ya kimaelezo. Utafiti huu ulibaini kwamba kunazo arki za utaifa katika nyimbo pendwa za Ken wa Maria kama vile utambulisho wa kiuana na kijamii, utamaduni, historia na ikolojia. Utafiti zaidi unaweza kufanywa kuhusiana na mada hii hasa jinsi wasanii wengine kutoka jamii ya Akamba wanavyotalii suala la ujenzi wa utaifa wa jamii.enUtaifaTaifaUtaifa wa KijamiiArki za UtaifaNyimbo PendwaUtamaduniUtambulishoArki za Utaifa wa Jamii ya AkambaArticle